Nimekuwa nikimfuatilia huyu jamaa anaitwa Daylan Page huko TikTok ambaye ni content Creator aki-deal na kutoa habari mbalimbali kuhusu matukio makubwa Ulimwenguni. Huyu jamaa page yake ilikuwa na wafuasi zaidi ya Milioni 15 na ndio page ya habari iliyokuwa na wafuasi wengi zaidi nyuma ya Daily Mail iliyokuwa na wafuasi zaidi ya Milioni 21.
Siku chache zilizopita kama siku 2 hivii page yake ilifungiwa na TikTok kwa sababu ya kukiuka sheria za TikTok ( TikTok Violation Policy) na taarifa ya kufungiwa kwa Account yake walioripoti wa kwanza ni DailyMail.
Sasa nikawa najiuliza kumbe hata Verified Account huwa zinafungiwa bila ya mtu kupewa taarifa!, Baada ya kupitia kwenye vyanzo mbalimbali ikasemekana kuwa Dylan Page sababu ya kufungiwa page yake ni baada ya Account yake kuripotiwa na DailyMail kwa TikTok ifungiwe sababu wanazijua wenyewe.
Vita vya kiushindani kupandisha habari mapema kati ya DailyMail na Dylan Page vita vyao vimekuwa kwa muda mrefu huku huyu jamaa akionekana kama anawapiga gap kwenye kuripoti matukio kitu ambacho kimejenga chuki kati yao.
Sasa siku ya leo Account ya Dylan Page imerudi tena na amerikodi Video akitaja wazi wazi kwamba vita vimerudi upya na safari hii vitachukua sura mpya kwani amegundua kuwa waliosababisha Account yake ifungwe ni hao DailyMail.
Chakumtenga mtu na mafanikio yake ni kifo tu, na Mungu .
Naamini atainuka imara maradufu zaidi👏
🙏🙏
Hiii Ni Hatari Sana
😃😃