Washington, D.C. – Ikulu ya Marekani ‘White House’ imetangaza nembo yao mpya, ikionyesha kurudi kwa Rais Donald Trump. Nembo hii inachukua nafasi ya muundo ulitumika wakati wa utawala wa Rais Joe Biden, na inatarajiwa kuleta mabadiliko katika utambulisho wa kipekee wa jengo hilo maarufu.
Kila utawala unapoingia madarakani, huwa na desturi ya kuunda tafsiri yake mwenyewe ya nembo ya White House, ikilenga kuwasilisha ujumbe wa kipekee na wa kiutawala. Nembo mpya ya Trump inajumuisha mistari iliyosafishwa na kuonesha kwa ujasiri bendera ya Marekani, ikionyesha dhamira ya utawala wake.
Wataalam wa masuala ya kisiasa wamesema kuwa nembo hii mpya inaweza kuwa ishara ya mabadiliko makubwa katika sera na mtindo wa uongozi wa Trump, huku ikitazamiwa kuathiri jinsi utawala wake utavyojulikana katika historia.


