Haki za Muziki wa Notorious B.I.G zauzwa Bilioni 389.9

Erry Mars
1 Min Read

Mkataba na haki za muziki wa rapa maarufu The Notorious B.I.G. umeuzwa kwa kampuni ya Primary Wave kwa thamani ya takriban dola milioni 150 sawa na Tsh Bilioni 389.9, kulingana na ripoti kutoka The Hollywood Reporter.

Mkataba huo unajumuisha haki za muziki wa Biggie, jina lake, na sura yake, na unatarajiwa kuwa moja ya makubaliano muhimu zaidi katika historia ya hip-hop.

Kuuzwa kwake kunakuja siku chache baada ya kifo cha mama yake, Voletta Wallace, ambaye alikuwa akisimamia mali yake tangu kifo chake mwaka 1997. Mkataba huu unatarajiwa kuwa mmoja wa muhimu zaidi katika historia ya hip-hop, Utaleta faida kubwa kwa Primary Wave, mashabiki wa Biggie wakiendelea kufurahia muziki na urithi wa rapa huyu ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 24.

Share This Article
1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!